Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tajuma ya Shirika la Habari la Hawza, katika mlipuko wa bomu mwaka 2005 nchini Uingereza, polisi wa nchi hiyo walitangaza kuwa kulikuwa na milipuko minne ya mabomu iliyofanyika jijini London, ambapo watu 52 waliuawa na zaidi ya 700 walijeruhiwa. Na katika kipindi cha siku tatu mfululizo baada ya tukio hilo, polisi waliripoti matukio 180 ya kigaidi dhidi ya Waislamu.
Utafiti wa maoni wa (The Guardian) unaonyesha kuwa takriban theluthi mbili ya Waislamu wa Uingereza walihamia nje ya nchi hiyo baada ya tukio hilo. Mhubiri mmoja wa kidini nchini Uingereza alitangaza kuwa:
kwa masikitiko makubwa, katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita, chuki dhidi ya Uislamu "Islamophobia" imeendelea kuongezeka nchini humo, miongoni mwa sababu kuu za hali hiyo ni kuongezeka kwa misimamo mikali ya kiitikadi, ugaidi, na sera za serikali zinazobagua Waislamu.
Aliongeza kwa kusema:
Sote tulishuhudia jinsi Bw. Jean Charles de Menezes, Mwingereza Muislamu mwenye asili ya Kibrazili, alivyonusurika katika mlipuko wa bomu wa tarehe 7 Julai, lakini baadaye alichukuliwa kimakosa na polisi wa London kuwa ni mshukiwa wa ulipuaji wa mabomu, na licha ya kuwa raia wa kawaida asiye na hatia, alipigwa risasi na kuuawa na polisi bila hata kuhojiwa!
Kwa mujibu wa taarifa ya Baraza la Waislamu wa Uingereza, nchi hiyo ni makazi ya jamii ya Kiislamu yenye mchanganyiko na utofauti mkubwa, ambapo wengi wao wana umri wa chini ya miaka 19. Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2021, asilimia 6.5 ya wakazi wa Uingereza, na takriban watu milioni 3.9 nchini Wales, ni Waislamu.
Shasta Gahir, mwanamke Muislamu, alisema katika mahojiano na "The Guardian" kwamba:
kama mwanamke Muislamu aliyezaliwa na kukulia Uingereza, madhila ya ubaguzi wa rangi daima yamekuwa sehemu ya maisha yake ya kila siku katika nchi hiyo.
Chanzo: The Guardian
Maoni yako